Kama huna Laki moja, TSA hapakuhusu

Dar es Salaam. Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limetangaza Agosti 26 kufanyika kwa uchaguzi mkuu  wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA) kwa ada ya Sh 100,000 kwa kila mgombea.

Leo Jumatatu, BMT imetangaza rasmi kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Chama hicho na tayari fomu za kugombea nafasi mbalimbali zimeanza kutolewa baada ya viongozi waliokuwa wakikaimu uongozi ndani ya TSA  kumaliza muda wao.

Ofisa Habari wa BMT, Frank Mgunga alisema uchaguzi huo utafanyika Agosti 26 jijini Dar es Salaam.

"Fomu zimeanza kutolewa hadi Agosti 20 kwa Sh 100,000 kwenye kila nafasi ya uongozi, mgombea atalipia benki kwenye akaunti ya Baraza na kuleta listi ya malipo hayo Baraza," alisema.

Nafasi zinazowania ni mwenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu Mkuu, mweka hazina, mkurugenzi wa ufundi na mkurugenzi wa Elimu na maendeleo.

 "Mgombea kwenye nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti lazima awe na historia ya kitaaluma, uadilifu na uwezo wa kukiwakilisha chama ndani na nje ya nchi.