Kaka atinga Milan kwa kishindo

Muktasari:

Kiungo huyo wa Brazil aliingoza klabu hiyo ya AC Milan kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa 2007

Milan, Italia. Mchezaji nguli wa AC Milan, Ricardo Kaka, ‘amerejea’ katika klabu hiyo kongwe Italia.

Kaka juzi alichomoza kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa San Siro, baada ya kutangaza kutundika daluga akiwa na klabu ya Orlando City ya Marekani.

Juzi alipata mapokezi makubwa katika mchezo ambao AC Milan iliichapa Vienna ya Austria mabao 5-1.

Mchezaji huyo bora wa zamani wa dunia, alitambulishwa wakati wa mapumziko mbele ya maelfu ya mashabiki wa klabu hiyo akiwa amevaa jezi ya timu hiyo.

Mtendaji Mkuu wa AC Milan, Marco Fassone amempa ofa Kaka kuwa Mkurugenzi wa Ufundi, lakini Mbrazil huyo hajaweka bayana kama amekubali au vinginevyo.

Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid alisema ni fahari kubwa kupewa ofa ya kuwa Mkurugenzi wa Ufundi AC Milan.