Kaheza achekelea Simba Day

Muktasari:

Kaheza anasema kazi ya soka inanoga kama  kuna mamia ya mashabiki, wanaounga mkono unachokifanya.

Dar es Salaam.Mshambuliaji mpya wa Simba,  Marcel Kaheza amesema anajisikia furaha kuwa miongoni mwa wachezaji watakaotambulishwa Simba Day, itakayofanyika Jumatano ya wiki hii.

Kaheza anasema kazi ya soka inanoga kama  kuna mamia ya mashabiki, wanaounga mkono anachokifanya.

"Unajua nilikuwa natamani wanavyofanyiwa wachezaji wa Simba siku ya Simba Day, kipindi ambacho

nilikuwa Majimaji ya Songea, niwe mkweli hakuna mchezaji asipenda thamani hiyo sema ni uchumi tu.

"Nikipata nafasi ya kucheza nimejipanga kuhakikisha natoa burudani mbele ya mashabiki wetu ambao watafika siku hiyo, tutakapocheza na Asante Kotoko," alisema Kaheza.