Maxime ana matumaini kibao

Muktasari:

Maxime anasema kuanza vibaya hakujamfanya akate tamaa na kuona ndio mwisho wa kikosi chao kuwania nafasi tatu za juu kama ilivyokuwa msimu uliopita hadi kupelekea kuibuka kocha bora.

LICHA ya kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime kutoanza vyema mwanzo wa msimu, lakini amejipa matumaini ya kurejesha heshima ligi itakapoanza baada ya kupisha michuano ya Challenji, iliyokuwa inafanyika Kenya.
Maxime anasema kuanza vibaya hakujamfanya akate tamaa na kuona ndio mwisho wa kikosi chao kuwania nafasi tatu za juu kama ilivyokuwa msimu uliopita hadi kupelekea kuibuka kocha bora.
"Bado safari ni ndefu, kikubwa naamini wachezaji watakuwa wamejua ni wapi waliteleza,tutanyenyuka na kuendelea na safari,lazima tutapambana ili kufika kwenye malengo yetu," anasema.
 Huku akisisitiza kwamba wachezaji wazuri na wenye viwango vya juu ni wale ambao wanakabiliana na changamoto ya ushindani, kitu anachosema kinawapa nafasi ya kuonekana ndani na nje.
"Si kuisaidia klabu tu, bali hata kupanua nafasi za ajira, nadhani kazi nzuri ni ile inayouzika kirahisi na sio mbovu, hilo litawafanya wajitume kwa bidii," anasema.