Kaduguda ‘Simba wa Yuda’ ajitosa Simba

Muktasari:

  • Kaduguda ‘Simba wa Yuda’ alisema amelitewa fomu na wanachama na kumuamuli aijaza kwa lengo la kuhakikisha wanamuona akiwa miongoni mwa wagombea wa nafasi hiyo.

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa zamani wa Simba, Mwina Kaduguda ameweka wazi kuwa jina lake ni miongoni mwa wanachama wa Simba wanaotarajia kuwania nafasi ya ujumbe katika uchaguzi wa Simba unaotarajiwa kufanyika Septemba 3 mwaka huu.

Kaduguda ‘Simba wa Yuda’ alisema amelitewa fomu na wanachama na kumuamuli aijaza kwa lengo la kuhakikisha wanamuona akiwa miongoni mwa wagombea wa nafasi hiyo.

"Nimeletewa fomu nyumbani na kuambiwa wamekuwa wakinifuata mara kwa mara kuniomba nigombee uongozi katika klabu yangu, lakini nimekuwa mgumu kufanya kwa sasa nimeamua kukubaliana nao kwasababu wameniambia endapo nitashindwa kufanya hivyo watajua mimi sio mwenzao huenda ni mpinzani wao wakimaanisha mimi nitakuwa ni Yanga," alisema Kaduguda.

"Siyo mara yao ya kwanza kufanya hivyo ata katika kipindi cha Avens Aveva pia walifanya hivyo, lakini nilikataa na wakanielewa lakini leo hii wamenigomea nimeamua kufanya hivyo kwa lengo la kukubaliana na wanachokiamini kutoka kwangu," alisema.

"Siyo wakati wa kampeni sasa naomba nisiongee mengi muda wa kampeni ukifika nitaongea mengi zaidi kwa sasa naomba niwaachioe wahusika waendelee na jukuimu lao la kutoa fomu," alisema Kaduguda.