KATIBA MPYA SIMBA: WAJUMBE SABA TU WANATOSHA BODI YA WAKURUGENZI

Muktasari:

Wajumbe saba waliochaguliwa na kuteuliwa kwa mujibu wa ibara ya 27 watakuwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi na watafanya kazi kwa mujibu wa kanuni zinazoongoza bodi ya wakurugenzi zilizoidhinishwa na Simba Sprts Cluba Company Limited

Dar es salaam. JANA Ijumaa tuliona jinsi mwanachama ambavyo anaweza kupata nafasi za kuongoza Simba kutokana na sifa inayotakiwa kwa mujibu wa Katiba yao.
Katiba ya Simba ambayo ni mpya baada ya kufanyiwa marekebisho imeelezea mambo mbalimbali ambayo mwanachama anapaswa kuyafuata ili kujua klabu yake inaongozwaje, leo Jumamosi tutaangalia jinsi Bodi ya Wakurugenzi itakavyokuwa inafanyakazi kutokana na muundo wake.

B. BODI YA WAKURUGENZI
Ibara ya 29: Muundo
1. Klabu ya Simba itafanya kazi chini ya Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Sports Club Company Limited.
2. Wajumbe saba waliochaguliwa na kuteuliwa kwa mujibu wa ibara ya 27 watakuwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi na watafanya kazi kwa mujibu wa kanuni zinazoongoza bodi ya wakurugenzi zilizoidhinishwa na Simba Sprts Cluba Company Limited.
3. Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi hawezi kuwa wakati huo huo mjumbe wa chombo cha haki cha klabu ya Simba au Kamati ya Uchaguzi.
4. Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi aliyechaguliwa na kuteuliwa kwa mujibu wa ibara ya 27 ya katiba hii atakoma kuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi iwapo atatenda au kufanya mojawapo ya mambo yafuatayo;
(a). Kujiuzulu kwa maandishi na kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa bodi ya wkaurugenzi
(b). Hatahudhuria mikutano minne mfululizo ya kawaida ya Bodi ya Wakurugenzi bila sababu za msingi.
(c). Anashindwa kutekeleza majukumu ya mjumbe kutokana na kuumwa au sababu nyingine yoyote kwa kipindi cha miezi 12 mfululizo.
(d). Kufariki.

Ibara ya 30. Muda wa madaraka wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi
1. Muda wa madaraka na mamlaka wa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi waliochaguliwa na kuteuliwa kwa mujibu wa ibara ya 27 ya katiba hii utakuwa miaka minene. Kamati ya muda (Interim Committes) hazitaruhusiwa.
2. Mamlaka ya wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi yanaweza kuongezwa muda na mkutano mkuu kwa sababu maalumu za msingi.
3. Endapo itatokea kuwa nafasi, yoyote ya bodi ya wakurugenzi kuwa wazi, katika mkutano mkuu wa kawaida unaofuata nafasi hizo zitajazwa kwa kuchaguliwa wajumbe wengine kwa kipindi kilichobaki cha mamlaka.

C. SEKRETARIETI
Ibara ya 31: Uanzishaji, Miundombinu na Kazi
1. Kutakuwa na sekretarieti yenye muundo wa ajira wa Simba Sports Club.
2. Wafanyakzi wote wa Sekretarieti watakuwa wa kuajiriwa na wataajiriwa na Bodi ya Wakurugenzi.
3. Sekretarieti itaundwa na
(a). Mkurugenzi wa wanachama na mashabiki
(b). Nafasi nyingine kama itakavyoamuliwa na Bodi ya Wakurugenzi
4. Sekretarieti itaongozwa na Mkurugenzi wa wanachama na mashabiki na kazi zake mahususi ni;
(a) Utekezaji wa maamuzi ya mkutano mkuu, bodi ya wakurugenzi na vyombo vingine vya Simba Sports Club Company Limited.
(b). Kufanya matayarisho ya mkutano mkuu.
(c). Kutayarisha kumbukumbu za mkutano mkuu
(d). Kuhakikisha usimamizi mzuri na utunzaji wa rasimali za Simba Sports Club.
(e). Kushughulikia mawasiliano ya Simba Sports Club na kusimamia ofisi za Simba Sports Club.
(f). Kutunza vitabu vya hesabu za Fedha za Simba Sports Club.
(g). Kushughulia mahusiano ya Simba Sports Club, wanachama wake na wadau wengine.

Ibara ya 32: Mkurugenzi wa wanachama na mashabiki
Kutakuwa na Mkurugenzi wa wanachama na mashabiki Simba Sports Club atakayesimamia sekretarieti ya Simba Sports Club.
1. Mkurugenzi wa wanachama na mashabiki atafanya kazi chini ya usimamizi na muongozo wa Mtendaji mkuu wa Simba Sports Club Company Limited.
2. Mkurugenzi wa wanachama na mashabiki atakuwa mwandishi wa mkutano mkuu na kuzihifadhi kumbukumbu hizo.
3. Mkurugenzi wa wanachama na mashabiki atawasimamia wafanyakazi wa Simba Sports Club na Utendaji wa sekretarieti.
4. Mkurugenzi wa wanachama na mashabiki atakuwa Ofisa Masuhuli wa klabu.
5. Mkurugenzi wa wanachama na mashabiki atapokea mipango na bajeti za kila mwaka kutoka Simba Sports Club Company Limited na kusimamia utekelezaji wake.

D. VYOMBO VYA HAKI
Ibara ya 33: Dhana
1. Simba Sports Club itatumia vyombo vya haki vya Simba Sports Club na Simba Sports Club Company Limited.
2. Vyombo vya haki vitakuwa ni Kamati ya Nidhamu na Kamati ya Madili. Vyombo hivi vitakuwa huru na maamuzi yake hayatangiliwa na chombo chochote cha Simba Sports Club.
3. Bila kuathiri maeneo ya mamlaka yaliyoandaliwa na mkutano mkuu, vyombo vilivyotajwa hapo juu vinaidhinishwa kuchukuwa hatua mbalimbali za nidhamu na maadili zilziotajwa katika katiba hii na kanuni zinazohusika.
4. Muundo, maeneo ya mamlaka, na kazi za vyombo vya haki, vitakuwa kwa mujibu wa kanuni mahususi ambazo lazima ziidhinishwe na Bodi ya Wakurugenzi.
5. Wajumbe wa vyombo vya haki watateuliwa na Bodi ya Wakurugenzi.


4. Kamati inaweza kutangaza hatua za kinidhamu zilivyoelezwa katika katiba hii au kanuni zilizotayarishwa kutokana na Katiba hii dhidi ya wanachama, wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi waliochaguliwa kwa mujibu wa ibara ya 26(8) au wafanyakazi wa Simba Sports Club.
5. Rufaa yoyote dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Nidhamu ya Simba Sports Club Company Limited, itapelekwa kwa kamati ya rufaa ya nidhamu ya TFF. Rufaa dhidi ya maamuzi ya TFF yanaweza pia kukatiwa rufaa CAS ambayo itakuwa na maamuzi ya mwisho.

Ibara ya 36: Kamati ya Maadili
1. Simba Sports Club inatambua Kamati ya Maadili ya Simba Sports Club Company Limited, itakayokuwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe watatu watakaoteuliwa na Bodi ya Maadili lazima wawe na taalumu ya sheria.
2. Chombo hiki kitasimamia Katiba ya Simba Sports Club kwa kutumia Kanuni zake za Maadili au Kanuni za TFF pale ambapo kanuni za Maadili za Simba Sports Club Company Limited hazipo.
3. Kamati itapitisha uamuzi iwapo angalau wajumbe watatu wamehudhuria mmojawapo akiwa Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti.
4. Kamati inaweza kutangaza hatua za kimaadili zilivyoelezwa katika Katiba hii au kanuni zilizotayarishwa kutokana na katiba hii dhidi ya wanachama, wajumbe wa bodi ya wakurugenzi waliochaguliwa kwa mujibu wa ibara ya 26 (8) au wafanyakazi wa Simba Sports Cluba.
5. Rufaa yoyote dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Simba Sports Cluba Company Limited itapelekwa kwa Kamati ya rufaa uya Maadili ya TFF. Rufaa dhidi ya maamuzi ya Kamati ya Rufaa ya Maadoli ya TFF yanaweza pia kukatiwa rufaa CAS ambayo itakuwa na maamuzi ya mwisho.

E. KAMATI YA UCHAGUZI
Ibara ya 37: Uanzishaji, Kazi na Majukumu
1. Kutakuwa na Kamati ya Uchaguzi wa Simba Sports Club itakayoteuliwa na Bodi ya Wakurugenzi ambayo itahusika na kuandaa na kusimamia uchaguzi wa Simba Sports Club, itashauri bodi ya wakurugenzi kuhusiana na kanuni za uchaguzi. Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club itafanya kazi chini ya usimamizi na maelekezo ya Kamati ya uchaguzi ya TFF.
2. Kamati ya cuhaguzi itaundwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe watatu. Mwenyekiti na Makamu wa Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi lazima wawe na taaluma ya sheria.
3. Kamati ya uchaguzi ya Simba Sports Club itatekeleza majukumu yake kwa kutumia kanuni za uchaguzi za Simba Sports Club na kama hazipo kanuni za uchaguzi za TFF zitatumika.
4. Kamati ya uchaguzi ya Simba Sports Club itapitisha maamuzi iwapo angalau wajumbe watatu wamehudhuria mmoja wao akiwa Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti.
5. Maamuzi ya Kamati ya uchaguzi ya Simba Sports Club yanaweza kukatiwa rufaa kwa kamati ya Rufaa ya uchaguzi ya TFF ambayo maamuzi yake yatakuwa ya mwisho.

F. BARAZA LA WADHAMINI
Ibara ya 38: Muundo wa mamlaka
1. Simba Sports Club itakuwa na Baraza la Wadhamini litakalokuwa na wajumbe wanne na ndiyo watakuwa wasimamizi na wadhibiti wa mali zote za klabu zinazohamishika na zisizohamishika na watunzaji wa 'lakiri' (seal) ya klabu.
2. Wajumbe wa Baraza la Wadhamini watateuliwa na Bodi ya Wakurugenzi na kuthibitishwa na Mkutano mkuu na kuanza kazi mara watakaposajiliwa na Kabidhi Wasihi mkuu wa Serikali. Mkutano mkuu ndio utakuwa na mamlaka ya kumuondoa mjumbe/wajumbe wa Baraza la Wadhamini toka kwenye wadhifa huo baada ya kupata taarifa toka Bodi ya Wakurugenzi.
3. Wajumbe wa Baraza la Wadhamini ndio watakuwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba Sports Club Holding Company Limited.
4. Baraza la Wadhamini litamiliki 99% ya hisa za Simba Sports Club Holding Company Limited kwa niaba ya Simba Sports Club na Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini atamiliki 1% ya hisa za Simba Sports Club Holding Company Limited kwa niaba ya Simba Sports Club.

Ibara ya 39: Ukomo wa Wadhamini
(a). Kufa, Kujiuzulu, kupata maradhi ya akili, kufungwa jela/magereza.
(b). Kuvuliwa nyadhifa na mkutano mkuu
(c). Bodi ya Wakurugenzi itawasilisha katika mkutano mkuu pendekezo la kumuondoa/kuwaondoa wadhamini watakaobainika ni chanzo cha migogoro ndani ya klabu au kama bodi ya wakurugenzi itakavyoona inafaa vinginevyo kwa maslahi ya klabu.

G. MATAWI YA SIMBA SPORT CLUB NCHI NZIMA
Ibara ya 40: (1) Matawi ya Simba Sprts Club na kazi zake
(a). Kutakuwa na uongozi wa matawi, wilaya na mikoa nchi nzima
(b). Matawi yote ya Simba Sports Club watalipa ada ya uanachama kila mwaka kwa kiwango kitakachopitishwa na MKutano Mkuu baada ya mapendekezo ya Bodi ya Wakurugenzi.
(c). Kila tawi litaruhusiwa kuwa na wanachama hai wasiozidi 250 na wasiopungua 50.
(d) Kila tawi litafanya uchaguzi wa uongozi wake utakaohusisha Mwenyekiti wa Tawi, Makamu Mwenyekiti wa tawi, Katibu mkuu wa tawi, Mweka Hazina na wajumbe watatu, mmoja kati yao awe mjumbe mwanamke ambao kwa ujumla wao ndio wataunda Kamati ya Utendaji ya tawi.
Itendelea.....................