Juve yabariki Barca kumnasa Dybala, kurithi Neymar

Roma, Italia. Kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri amesema hana wasiwasi wa kumpoteza kiungo wake Paulo Dybala nayetakiwa na Barcelona kuziba pengo la Neymar.

Kama Neymar ataondoka Barcelona na kuhamia Paris Saint-Germain msimu huu, miamga hiyo ya Hispania iweka wazi itageukia kwa kiungo wa Juventus, Dybala.

Kuna mambo mawili ambayo yatasababisha nyota huyo wa Brazil kuondoka kwanza ni PSG kufikia gharama ya euro 222 milioni ya kununua mkataba wa kumwachia kutoka Barca.

Jambo la pili ni kuwa Neymar anataka mshahara wake ulingane na Lionel Messi, jambo ambalo klabu hiyo haiwezi kufanya kwa muda huu.

Kama itatimia kweli na Neymar ataondoka Camp Nou kwenda Parc des Princes msimu huu basi Barcelona itaziba pengo kwa Dybala.

"Sina wasiwasi na kumpoteza Dybala," alisema Allegri, katika mkutano na wanahabari wakizungumzia mechi yao ya kirafiki dhidi ya Barca.

"Katika upande mwingine sijui nini kinachoendelea kati ya Neymar na PSG, kwa hiyo sijui kama hiyo inaweza kuwa sababu ya Barcelona kuhitaji kununua mchezaji wa kuziba pengo lake.

"Hicho ni kitu ambacho siwezi kukizuia kwa hiyo sina hofu yoyote kwa hilo."