Julio ajivunia kumfundisha Samatta

Muktasari:

  • Julio anatarajiwa kuisimamia timu ya Samatta katika mchezo wa hisani hapo kesho Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, dhidi ya timu ya Alikiba.

Dar es Salaam. Kocha mwenye maneno mengi, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amejivunia kumfundisha nyota wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta wakati akiwa katika kikosi cha vijana cha Simba.
Julio anatarajiwa kuisimamia timu ya Samatta katika mchezo wa hisani hapo kesho Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, dhidi ya timu ya Alikiba.
"Usikivu wake ndio siri ya mafanikio. Sipendi kujisifia ila nafurahia kumfundisha Samatta wakati akiwa Simba kwenye timu ya vijana.
"Binafsi nampongeza sana, Samatta pamoja na vijana wenzake kwa hili ambalo wanaenda kulifanya kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu," alisema Julio.
Mchezo huo wa hisani utachezwa kuanzia majira ya saa 9:0 alasiri ili kuwapa muda wadau wa soka ambao watakuwa wameifunga kuwahi makwao kufuturu.