Jezi za Kagere, Salamba habari ya mjini Arusha

Muktasari:

Viingilio katika mchezo Simba na Arusha Utd vitakuwa 20,000 VIP A’, 10,000 VIP B’ na 5,000 kwa mzunguko

Arusha: Saa chache kabla ya mchezo wa kirafiki kati ya Simba Sc na Arusha United, tayari jezi za mastaa wa mabingwa wa ligi kuu Bara Simba Sc zimeanza kuuzwa katika mitaa mbalimbali ya jiji la Arusha.

Licha ya kuwepo kwa mastaa wengi katika timu hiyo, lakini jezi ya Adam Salamba pamoja na Meddie Kagere ndio zimekuwa Habari ya mjini katika viungo vya uwanja.

Hata hivyo; wauzaji jezi wamesema licha ya changamoto kubwa ni kupata jezi hizo za wachezaji hao wapya.

Pamoja na wakali hao pia jezi za Pascal Wawa nayo imeonekana ikitawala kama ilivyokuwa ya Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya ambao walikua na timu hiyo tangu msimu uliopita.