Jezi ya Tshishimbi, Ajib, Chirwa zageuka dili Singida

Muktasari:

Yanga inajiandaa na mchezo war obo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Singida United utakaochezwa Jumapili hii

Singida. Jezi ya Papy Tshishimbi, Ibrahimu Ajib na Obrey Chirwa zimetawala katika mitaa ya mji wa Singida kwa wafanyabiashara ndogondogo kuwauzia mashabiki wa timu hiyo.

Yanga ipo mjini Singida ikijiandaa na mchezo wake wa robo fainali Kombe la FA dhidi ya Singida United utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Namfua.

Jezi moja ya Tshishimbi imepanda kutoka Sh 5000 hadi 7000 wakati ili ya Ajib na Chirwa zenyewe zimefikia Sh6000 kutoka Sh 5000 ya sasa.

Asilimia kubwa ya wafanyabiashara hizo, wameanza kujisogeza kwenye uwanja wa Namfua tayari kutafuta riziki zao kufuatia kuwasilia kwa Yanga.

Miongoni mwa wafanyabiashara wanaofurahia wiki hii ya ujio wa Yanga ni wauza jezi ambao wadai mauzo yamepanda karibu mara tano ya kiwango cha kawaida.

Mfanyabiashara Ally Ngassa alisema jezi inayoongozwa kwa kununulika zaidi ni Tshishimbi wengine ni Ajibu na Chirwa wanamfuatia katika kununuliwa kwa wingi.

"Amekuwa kipenzi cha watu wa Singida ambao wanaipenda Yanga, pia hata watu wa mikoani ambao wameanza kufika kushuhudia mechi nao wanaonekana kuvutiwa naye," alisema Ngassa.

Mama lishe wao wamedai kujipanga kuongeza kiwango cha mapishi yao ili kukidhi idadi kubwa ya wapenzi wa soka wanaoendelea kuja kutoka mikoa ya jirani.