JB: Tulichelewa kumtumia Mzee Majuto

Muktasari:

Akizungumza katika viwanja vya Karimjee, JB amesema pamoja na yeye kucheza naye filamu mbili, ikwemo Shikamoo Mzee, Nakwenda kwa mwanangu, bado hawakimtumia vilivyo.

Dar es Salaam. Mcheza filamu Jacob Steven ‘JB’ amesema walichelewa kumtumia mzee Majuto kutokana na kipaji alichokaliwa.
Akizungumza katika viwanja vya Karimjee, JB amesema pamoja na yeye kucheza naye filamu mbili, ikwemo Shikamoo Mzee, Nakwenda kwa mwanangu, bado hawakimtumia vilivyo.
Amesema Mzee Majuto ambaye ameigiza miaka mingi bado walikiwa hachoshi machoni mwa watu na ndio maana hata akitoa filamu kwa mfululizo bado zilifanya vizuri.
JB amesema kupitia kifo chake amejifunza mengi ikiwemo kuipenda sanaa kama kazi kwani ndizo zilizomfanya akapata mafaniko mbalimbali ikiwemo ya kufanya matangazo.
"Mzee Majuto ametufundisha kwamba tukiijeshimu kazi ya filamu tunaweza kuwa na mafanikio mengi kuliko tunavyofikiria na kubaki kulalamika kila siku, kwani vitu vingi alivyokuwa akivimiliki vya maendeleo vimetokana na Sanaa hii," amesema JB.