Izzo aamua kutoa albamu kuwafukuzia Navy Kenzo

Muktasari:

Rapa anaetamba na ngoma ya Rafiki aliyomshirikisha msanii mwenza toka kundi lao la pamojaThe Amaizing ametangaza ujio wa albamu yake mpya kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Wakati wasanii wengi wakiogopa kutoa albamu, rapa anayewakilisha Mkoa wa Mbeya amesema yeye haogopi na yuko tayari kuwafuata Navy Kenzo waliochia albamu yao mwaka huu.
Rapa anaetamba na ngoma ya Rafiki aliyomshirikisha msanii mwenza toka kundi lao la pamojaThe Amaizing ametangaza ujio wa albamu yake mpya kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Katika moja ya mahojiano Izzo alikiri kuja kwa albamu hiyo lakini bado hajaweka wazi wasanii ambao watu wategemee kuwakuta katika albamu huku akisema si muda atatangaza kila kitu.
“Nakuja na albamu kabla ya mwaka huu,kuhusu wasanii ambao watakuepo na mambo mengine si muda nitasema na mambo mengi ila sasa watu wategemee albamu hiyo,” alisema
Izzo kwa siku za karibuni amekua akitoa kazi mbalimbali, akiachia kazi mbili kutokea kundi lake The Amaizing ambazo ni Dangerous Boy pamoja na Balaa huku akiachia kazi zingine kama Tumeoana,Umeniweza pamoja na sasa Rafiki inayofanya vizuri ambapo mpaka sasa Youtube imetazamwa na watu zaidi 70,000.