Ivo Mapunda awaibukia wababa!

Muktasari:

Mapunda ambaye kwa sasa anaendeleza kituo chake cha kuendeleza vijana wadogo kwenye soka kilichopo Kitunda jijini Dar es Salaam cha Ivo Mapunda Sports Center.

Dar es Salaam. Mlinda mlango wa zamani wa Simba, Yanga na Azam FC, Ivo mapunda amewapa ushauri wa bure wanaume kuwa na mapenzi na familia zao hasa watoto wanao wazaa.

Mapunda ambaye kwa sasa anaendeleza kituo chake cha kuendeleza vijana wadogo kwenye soka kilichopo Kitunda jijini Dar es Salaam cha Ivo Mapunda Sports Center.

Amesema, wanaume au wababa, wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika malezi kama wanavyofanya sehemu kubwa ya wanawake.

"Sehemu kubwa ya wakina mama (wanawake) mara nyingi ndiyo wameonekana kuwa mtari wa mbele katika malezi na wasimamizi wa familia,ninacho waambia wanaume wenzangu tubadilike na kuwa mfano,"alisema Mapunda.

Amesema, kwa nafasi yake kama baba amekuwa mstari wa mbele kufanya hivyo na hupenda kuwaelezea vijana wadogo namna maisha yake yalivyokuwa mpaka sasa.