Yanga na Kakolanya kama kawa mwanangu

Muktasari:

Kakolanya amegoma kujiunga na Yanga iliyopo Kisiwani Zanzibar kutokana na madai yake hayo kwa klabu, lakini pamoja na hilo uongozi umepeleka jina lake katika mashindano hayo ambayo vijana hao wa Jangwani wataiwakilisha Tanzania Bara kwenye  Ligi ya Mabingwa Afrika.

NYOTA njema  za mlinda mlango wa Yanga, Beno Kakolanya kulipwa pesa za usajili na klabu yake, zimeonekana baada ya jina lake kuwa miongoni mwa yaliyopelekwa CAF.
Kakolanya amegoma kujiunga na Yanga iliyopo Kisiwani Zanzibar kutokana na madai yake hayo kwa klabu, lakini pamoja na hilo uongozi umepeleka jina lake katika mashindano hayo ambayo vijana hao wa Jangwani wataiwakilisha Tanzania Bara kwenye  Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katibu wa Yanga,  Boniface Mkwasa amesema, wako mbioni kumlipa mchezaji huyo haki zake zote: "Kwani michuano inaanza leo, si bado kuna muda."
Kakolanya ni miongoni mwa makipa watatu wa Yanga, wengine ni Mcameroon Youthe  Rostand na Ramadhan Kabwili.
Kwa upande wa Kakolanya kuhusu taarifa ya jina lake kupelekwa CAF na ana mpango gani amesema:  "Kwa sasa siwezi kuwa msemaji, waliopeleka wanajua taratibu zote cha msingi naendelea kujifua na mazoezi binafsi."