Ibrahimovic kutua mazoezini kuiongezea nguvu Man United

Muktasari:

  • Zlatan ambaye ameimarika afya yake baada ya kuwa majeruhi kwa kipindi kirefu tangu kumalizka kwa msimu uliopita, anatarajiwa kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji.

 Mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic anatarajiwa kutua London muda wowote kuanzia sasa ili kujiunga na kikosi hicho.

Zlatan ambaye ameimarika afya yake baada ya kuwa majeruhi kwa kipindi kirefu tangu kumalizka kwa msimu uliopita, anatarajiwa kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji.

Mchezaji huyo mwenye miaka 35, alishauriwa na madakari wake kutokuwa na haraka ya kurudi dimbani kutokana na hofu ya kutemwa klabuni hapo.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kwamba tayari ameshatengewa mkataba na kinachosubiriwa ni kuusaini ndani ya miezi michache ijayo.