Ibrahimovic kupewa majukumu ya ukocha Manchester

London, England. Mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic (35) anatarajiwa kukabidhiwa majukumu mapya  akikamilisha kusaini mkataba wake na Manchester United.

Taarifa zilizopatikana klabuni hapo imeelezwa kwamba Kocha Jose Mourinho amepanga kumpa majukumu ya kufundisha kikosi hicho ili kuendelea kuwa na timu tishio msimu huu.

Raia huyo wa Sweeden amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha yaliyokuwa  yakimkabili baada ya kupata majeraha wakati wa michuano ya Ligi ya Europa msimu uliopita.