Huyu Mwantika mbona yuko fresh

Muktasari:

Daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa alitoa ufafanuzi kwamba Mwantika hana tatizo la moyo kama ilivyoelezwa awali ambapo alisema amefanyiwa vipimo vya kina katika tasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete.

BEKI wa Azam FC, David Mwantika kwa sasa yupo fiti kucheza mechi zilizobakia baada ya kuzimia timu yake ilipokuwa imecheza na Mtibwa Sugar.

Daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa alitoa ufafanuzi kwamba Mwantika hana tatizo la moyo kama ilivyoelezwa awali ambapo alisema amefanyiwa vipimo vya kina katika tasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete.

“Majibu ya awali ilikuwa ni mchezaji huyo ana matatizo ya moyo, lakini baada ya vipimo vya kina ameonekana kuwa hana tatizo,baada ya kutoka nilianza kumpa mazoezi ya hatua na sasa kajiunga na timu,” alisema.

Kwa upande wa kocha msaidizi wa timu hiyo, Iddy Cheche alisema Mwantika amepona na anaweza akacheza mechi mojawapo zilizobakia kumalizia msimu wa 2017/18.

Alisema kuwa ni uamuzi wa mwalimu kama atahitaji huduma yake kwa sasa.

“Itategemeana na umuhimu ambao atahitajika, lakini yupo vizuri na sasa anafanya mazoezi ya kujiweka fiti, kutokana na muda ambao alikaa nje ya kazi,” alisema.