Huyo Ajib usipime huko Taifa

Muktasari:

Ajib alikosekana muda mrefu katika kikosi chake cha Yanga baada ya kusumbuliwa na matatizo ya kifamilia, lakini kuibuka kwake uwanjani kumeanza kutoa matumaini katika kikosi chake cha Jangwani.

Dar es Salaam. Mshambuliaji Ibrahim Ajib anayekipiga katika kikosi cha Yanga, ameibukia katika mechi maalumu ya Timu Kiba dhidi ya Timu Samatta, mchezo wenye nia ya kuchangidha fedha kwaajili ya kuchangia elimu kwa shule ya msingi.

Ajib alikosekana muda mrefu katika kikosi chake cha Yanga baada ya kusumbuliwa na matatizo ya kifamilia, lakini kuibuka kwake uwanjani kumeanza kutoa matumaini katika kikosi chake cha Jangwani.

Ajib katika mchezo huo ambapo alikuwa akiichezea Timu Kiba, aliweza kuifungia timu hiyo mabao mawili, hali ambayo mashabiki walianza kuhoji juu ya kiwango chake.

Licha ya kukosekana muda mrefu katika kikosi chake cha Yanga, bado ameonekana kuwa na uwezo wake ule ule huku staili yake ya uchezaji ikionekana kuimarika zaidi.