Huko Mtwara nako kumenoga

Muktasari:

  • Huko Newala kuna mashindano ya Dotto Super Cup yalianza kufanyika mwezi uliopita ambazo sasa ni timu tatu zimetinga hatua ya 32 bora huku yakichezwa kwa mtoano ambazo ni Newala Veteran, Nakachela Stars na Magu Stars wakati Satari FC, Gibrota FC na Super Stars.

NYANDA za Kusini inawakilishwa na timu moja pekee kwenye Ligi Kuu Bara ambayo ni Ndanda lakini pia kuna Namungo ya Daraja la Kwanza ila sasa wadau wa kanda hiyo wameamka ili kusaka vipaji kwa kuanzisha mashindano mbalimbali itakayowasiadia kupata vijana watakaocheza soka hatua za juu.

Huko Newala kuna mashindano ya Dotto Super Cup yalianza kufanyika mwezi uliopita ambazo sasa ni timu tatu zimetinga hatua ya 32 bora huku yakichezwa kwa mtoano ambazo ni Newala Veteran, Nakachela Stars na Magu Stars wakati Satari FC, Gibrota FC na Super Stars.

Katika ratiba yao inaonyesha kwa mashindano hayo yataendelea kesho Ijumaa ambapo kutakuwa na mechi moja Magereza FC watacheza na Abajalo FC Uwanja wa Shule ya Msingi Twende Pamoja.

Mkurugenzi wa michuano hiyo ambayo kwa asilimia kubwa imekusanya vijana kutoka mtaani, Joseph Dotto aliliambia Mwanaspoti kuwa lengo lao ni kuinua soka kwa vijana ambapo watapata nafasi ya kucheza timu zingine na kupata ajira.

“Sio kwamba tumelenga kuwapa zawadi pekee, bali ni hata kuwatengenezea njia ya kupita kufikia mafanikio kwa njia ya soka.

“Kuna baadhi wanaoweza kuonyesha kiwango cha juu wanaweza kupata timu kwa uharaka na wengine watapambana zaidi.

“Kupitia mashindano haya mkoa wa Mtwara utakuwa na wachezaji wengi kwenye timu zinazocheza ligi madaraja ya juu kwamba watawatumia vijana wao wenyewe na kupunguza gharama la usajili wa gharama kubwa,” alisema Dotto.

Mkoa huo pia ulikuwa ukijivunia timu ya Bandari iliyotikisa Ligi Kuu na kutoa wachezaji kadhaa akiwemo Idelfonce Amlima ambaye alikuja kutamba.