Hilo Chama la Wana limewanasa wakali tisa

Muktasari:

  • Chama la Wana liliyumba msimu uliopita katika Ligi Kuu Bara kutokana na kukosa fedha, sasa imemsainisha Muwonge mkataba wa mwaka mmoja akiwa sehemu ya nyota watakaoichezea timu hiyo katika ligi ya msimu mpya.

KLABU ya Stand United ‘Chama la Wana’ kweli limedhamiria baada ya kunasa wachezaji wapya tisa, ikiwamo kumwongezea mkataba kipa wake Mganda, Frank Muwonge.

Chama la Wana liliyumba msimu uliopita katika Ligi Kuu Bara kutokana na kukosa fedha, sasa imemsainisha Muwonge mkataba wa mwaka mmoja akiwa sehemu ya nyota watakaoichezea timu hiyo katika ligi ya msimu mpya.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya timu hiyo, Geoffrey Tibakenda, amewataja wachezaji hao tisa waliosajiliwa sambamba na kuongezewa mkataba kwa Mganda huyo kuwa ni Ambrose James, David Mwita, John Mwenda, Emmanuel Kitoba, Ally Hamad, Makenzi Kapinga, Mageta Paul, Mathias Charles na Morris Machela.

Pia alisema sasa wamebakzia nafasi nne ambazo wataangalia zaidi washambuliaji.

“Tutafanya hivyo ingawa pia tunahitaji beki na kiungo,” alisema Tibakenda.

Chama la Wana liliyumba kiuchumi baada ya waliokuwa wadhamini wao Kampuni ya Acacia kusitisha mkataba wa udhamini kutokana na mzozo ambao baadaye ulikwenda kumalizwa mahakamani.