Hii kali:Guardiola miaka10, mataji 24

Muktasari:

Msimu yake miwili ndani ya Manchester City, amesghatwaa mataji matatu Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Ligi.

London, England. Nyota ya Kocha Pep Guardiola imezidi kung’ara wakati kocha huyo anapotimiza miaka kumi tangu ajitose kwenye ukocha baada ya jana kuiwezesha Manchester City kutwaa Ngao ya Jamii.

Guardiola ametimiza mataji 24 tangu alipotundika daluga na kugeukia ukocha, ingawa alianza kazi hiyo kwa vibaya kwa Barcelona kuchapwa na Numancia na kufuatiwa na sare dhidi ya Racing.

Kocha huyo amekuwa na mafanikio kwa kila Klabu anayoiongoza misimu minne aliyoinoa Barcelona alitwa mataji 14, matatu ya LaLiga, mawili ya Kombe la Ligi, matatu ya Spanish Super Cups, mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mawili ya European Super Cups na mawili ya Klabu Bingwa ya Dunia.

Katika misimu mitatu aliyoinoa Bayern Munich ya Ujerumani alitwaa mataji saba matatu ya Bundesliga, mawili ya Kombe la Ligi, moja la European Super Cup na moja la Klabu Bingwa ya Dunia.

Msimu yake miwili ndani ya Manchester City, amesghatwaa mataji matatu Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Ligi.

Ndani ya City taji pekee analolisaka ni lile la Ligi ya Mabingwa Ulaya ambalo klabu hiyo haijawahi kulitwaa mara ya mwisho klabu hiyo kutwaa taji la Ulaya ni msimu wa mwaka 1969/70 walipotwaa Kombe la Washindi.