Hatimaye Klopp atimiza ahadi kumyakua Alisson

Muktasari:

Kipa huyu alikuwa chaguo namba moja la Brazil katika michuano ya kombe la dunia nchini Russia mbele ya kipa wa Manchester City, Ederson.

Hata hivyo si wengi wanaomfahamu vema Alisson. Ni huyu Alisson?

ROME, ITALIA. HATIMAYE Liverpool wamevunja rekodi ya uhamisho wa makipa duniani kwa kulipa kiasi cha pauni 67 milioni kwa kipa wa AS Roma na timu ya taifa ya Brazil, Alisson Becker.

Kipa huyu alikuwa chaguo namba moja la Brazil katika michuano ya kombe la dunia nchini Russia mbele ya kipa wa Manchester City, Ederson. Hata hivyo si wengi wanaomfahamu vema Alisson. Ni huyu Alisson?
Jina lake kamili ni Alisson Ramses Becker na alizaliwa Okotoba 2, 1992 katika mji wa Novo Hamburgo nchini kwao Brazil. Alianza kucheza soka katika shule ya soka ya klabu maarufu ya Nacional akiwa na umri wa miaka 10 mnamo mwaka 2002.
Baada ya kuendelea kukomaa hatimaye alijiunga na kikosi cha chini ya umri wa miaka 23 kabla ya kucheza mechi ya kwanza katika kikosi cha wakubwa mnamo Februari 17, 2013. Alianza katika pambano dhidi ya Cruizero micjhuano ya jimbo ambalo lilimalizika kwa sare ya 1-1.
Akacheza pambano lake la kwanza Ligi Kuu mnamo Agosti 25, 2013 wakati alipoanza katika sare ya 3-3 dhidi ya Goias. Katika msimu huo alikuwa alikuwa chaguo la pili kwa kaka yake, Muriel ambaye alikuwa kipa wa kwanza. Yeye alikuwa anapambana na kipa wa pili Agenor. Alimaliza msimu akiwa amecheza mechi sita za kikosi cha kwanza.