Hapa Chuji, kule Boban hapatoshi Uhuru kesho

Muktasari:

  • Wawili hao wamewahi kucheza pamoja Simba kabla ya Chuji kutimkia Yanga. Pia wanakumbukwa kwa kitendo chao cha kufukuzwa kocha Marcio Maximo katika kambi ya Taifa Stars ikiwa katika mashindano ya CHAN2009 nchini Ivory Coast.

Dar es Salaam. Kiungo wa Coastal Union, Athuman Idd 'Chuji' atakuwa na kibarua kizito mbele ya rafiki yake Haruna Moshi ‘Boban’ wa African Lyon kesho Ijumaa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaa,

Chuji na Boban ni marafiki na wanasifikia kwa kuwa watoto watukutu wenye vipaji vikubwa, lakini kesho watakuwa na kazi ya kuthibisha ubora wao mbele ya mashabiki wao.

Wawili hao wamewahi kucheza pamoja Simba kabla ya Chuji kutimkia Yanga. Pia wanakumbukwa kwa kitendo chao cha kufukuzwa kocha Marcio Maximo katika kambi ya Taifa Stars ikiwa katika mashindano ya CHAN2009 nchini Ivory Coast.

Akiuzunguzia mchezo wa kesho Chuji alisema wanajua ugumu wa mechi za ugenini, lakini watapambana kupata matokeo mazuri.

"Tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo na wachezaji wote tuko vizuri tayari kwa mchezo.

"Mechi za ugenini ni ngumu sana lakini tutapambana kuhakikisha tunashinda au hata kupata sare tu kuliko kufungwa.

Chuji katika mchezo huo atapambana dhidi ya rafiki yake mkubwa Boban ambaye waliwahi kucheza wote Simba.