Gor Mahia yaitekenya Yanga mabao 4-0

Muktasari:

  • Mpaka  kipindi cha kwanza kinamalizika hapa katika uwanja wa Kasarani Nairobi katika mechi ya kundi 'D' kati ya Gor Mahia walikuwa mbele kwa mabao 2-0.

Timu ya Gor Mahia imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Kundi D na kuwafanya kufikisha alama 5 kwenye kundi hilo.
Mpaka  kipindi cha kwanza kinamalizika hapa katika uwanja wa Kasarani Nairobi katika mechi ya kundi 'D' kati ya Gor Mahia walikuwa mbele kwa mabao 2-0.
Mabao ya Gor yalifungwa na Jacques Tuyisenge dakika 22 ambapo aliwazidi ujanja mabeki wa kati wa Yanga na kumalizia pasi akiwa amebaki na kipa Youthe Rostand.
Gor ambao walionekana wapo vizuri katika kipindi cha kwanza kwa kushambulia mara kwa mara walipata bao la pili na la nne dakika ya (45,87) kupitia kwa Ephrem Guikan ambaye alimalizia pasi safi huku mabeki wa Yanga wakizani ameotea wakati bao la tatu lilikuwa la kujifunga zawadi kutoka kwa Haji Mwinyi.
Yanga walipoteza kipindi cha kwanza kwa walishindwa kufanya shambulizi lolote la hatari zaidi ya faulo ya Ibrahim Ajibu ambayo Juma Mahadhi alichezewa rafu nje ya boksi.
Faulo hiyo ya Ajibu haikuwa ya hatari kwani mpira aliopiga ulipaa juu ya goli la tangu hapo kulikuwa hakuna shambulizi lolote na mpaka dakika 45 zimalizika kipa wa Gor Mahia Shaban Odhoji alikuwa anaongea tu.
Yanga mbali ya kushindwa kufanya mashambulizi walikiwa wakipoteza mipira mingi kuanzia katika safu ya viungo na washambuliaji wao Ajibu,  Yohana Mkomola, Mahadhi na Buswita walikuwa kama wanatembea tu.
Viungo wawili wa Yanga Papy Kabamba Tshishimbi na Haji Mwinyi walizidiwa zaidi katika kukaba na kufanya viungo wa Gor Mahia kutamba kwa kupiga pasi nyingi za kushoto na kulia.
Hata mabao mawili ambayo walifungwa Yanga yalikuwa kutokukaba vizuri katika eneo la kiungo na kupigwa pasi mbili za maana ambayo Yanga walijikuta zinawazuru.
Yanga walizidiwa katika eneo la kiungo kwani Mwinyi ambaye alianza kama kiungo mkabaji alikuwa anashindwa kutimiza majukumu ipasavyo huenda ilikuwa hivyo kwa sababu kiasilia si nafasi yake.
Mwinyi Mara zote ilizoeleka akicheza kama beki wa kushoto lakini kocha wa Yanga Mkongomani Mwinyi Zahera alimuanzisha katika nafasi hiyo.
Mabeki wa Yanga haswa Andrew Vicente 'Dante' na Abdallah Shaibu walikuwa hawaelewani kwani hata mabao mawili waliofungwa kipindi cha kwanza hawakukaba mpaka mwisho na wafungaji kufunga bila ya kukabwa na beki yoyote.