Gary Neville amshangaa Danny Rose kuropoka siri za timu

Friday August 11 2017

 

England. Mchezaji wa zamani wa Manchester United, amemshukia mchezaji wa Tottenham, Danny Rose kutokana na mahojiano aliyoyafanya na kituo cha michezo SunSport na kuponda hatua ya klabu hiyo kutosajili msimu huu.

Licha ya kuwa mchezaji huyo alizungumzamambo ya kweli lakini jambo hilo limechukuliwa kwa mitazamo tofauti, huku akisema kikosi chao hakiwezi kujilinganisha na Manchester City na Chelsea.

Kocha Maurcio Pochettino msimu huu hajasajili mchezaji yeyote kutokana na uongozi wa klabu hiyo kutangaza kuwa fedha zote zimeelekezwa kwenye matengenezo ya uwanja.