Gareth Bale mbioni kufunga ndoa

MCHUMBA wa muda mrefu wake fowadi wa Real Madrid, Gareth Bale, kichuna Emma Rhys kadokeza kuwa ile harusi yao iliyoratibiwa kufanyika Desemba mwaka jana, itafanyika mwishoni mwa msimu huu wa ligi.


Kupitia posti kadhaa ambazo amekuwa akitupia  kwenye mitandao ya kijamii, Emma anaonekana kuashiria kuwa ndoa yao itafanyika Mei 2018 mara tu baada ya Ligi Kuu kufikia kikomo.
Harusi hiyo ilikuuwa ifanyike Desemba ya mwaka jana ila ikaahirishwa kwa sababu kadhaa wa kadhaa.


Sasa Emma ameweka bayana kwamba mwaka huu hautaisha kabla hajaitwa mke wa mtu. Wapenzi hao wamekuwa wapenzi kwa zaidi ya miaka 10 na kufanikiwa kujaliwa mabinti wawili.