Fabregas kuikosa Arsenal Jumamosi

Muktasari:

  • Kiungo huyo, 31, anasumbuliwa na goti na alikosa mechi ya Chelsea waliyoshinda mabao 3-0 dhidi ya Huddersfield Town Jumamosi iliyopita.

London, England. Cesc Fabregas ataikosa timu yake ya zamani ya Arsenal itakapokuwa ikicheza na Chelsea Jumamosi mechi ya Ligi Kuu England kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti.

Kiungo huyo, 31, anasumbuliwa na goti na alikosa mechi ya Chelsea waliyoshinda mabao 3-0 dhidi ya Huddersfield Town Jumamosi iliyopita.

Wachezaji wa Chelsea walikuwa kwenye mazoezi tangu Jumatatu, lakini Fabregas hakuwa kwenye timu hiyo iliyokuwa ikijifua kwenye Uwanja wa Stamford Bridge Jumamosi.

Maurizio Sarri alisema kuwa ahis o Premier League debutivyhilo haliwezi kuwa tatizo dhidi ya kikosi cha Unai Emery na huenda akapangwa Mateo Kovacic kuanza na mechi yake ya kwanza.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia, alijiunga na timu hiyo akitokea Real Madrid kwa mkopo lakini hakucheza mechi na Huddersfield na tayari amehakikishiwa namba katika kikosi cha Sarri dhidi ya Arsenal.

Mechi na Huddersfield, Sarri alisimamisha viungo watatu, Jorginho, N’Golo Kante na Ross Barkley kabla ya Ruben Loftus-Cheek kipindi cha pili

Arsenal, ina majeruhi, fulubeki wa kushoto, Ainsley Maitland-Niles ambaye alilazimika kutoka katika mechi ya kwanza waliyofungwa mabao 2-0 na Manchester City Jumapili.

Emery atamkosa Sead Kolasinac, wakati Nacho Monreal amerejea kuanza mazoezi katika kikosi hicho baada ya kuumia goti.