Nchimbi ajivunia changa twawala

Muktasari:

  • Njombe Mji kwa sasa ipo nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara

Mshambuliaji wa Njombe Mji, Ditram Nchimbi  amesema licha ya Simba kuwafunga mabao 4-0,  anaamini mabeki wa timu hiyo amewaachia uchovu wa kukabana naye.

Njombe Mji iliyopanda daraja msimu huu imekutana na kipigo kikali kutoka kwa Simba inayosaka ubingwa msimu huu.

Nchimbi kabla ya kujiunga na Njombe Mji, alikuwa na Mbeya City, ameeleza uzoefu wa namna ya kucheza na timu kongwe Simba na Yanga, huku akisema kikosi chao wengi ni wageni katika ligi.

" Nina uzoefu wa kukabilina na nyota wa Simba na Yanga kwa kuwa nimekutana nao mara kadha nikiwa  Mbeya City na kilichotuangusha ni kikosi chetu kuwa na wageni wengi kwenye ligi."

"Simba na Yanga mara nyingi zinabebwa na uzoefu, lakini asilimia kubwa wale ambao wametoka ligi daraja la kwanza, lazima waanze kufundishwa mifumo kwanza hadi wazoee inachukua muda kidogo," alisema Nchimbi.