Elneny aitosa Leicester akomaa Arsenal

Muktasari:

Arsenal ilikubali dau la pauni10milioni kwa ajili ya kuuza kiungo huyo Misri mwenye miaka 25, na kumruhusu kuzungumza na Leicester 'Foxes' kuhusu uhamisho wake.

London, England. Kiungo Mohamed Elneny amekataa kujiunga na Leicester City kwa sababu ya kupenda maisha ya jiji la London.

Arsenal ilikubali dau la pauni10milioni kwa ajili ya kuuza kiungo huyo Misri mwenye miaka 25, na kumruhusu kuzungumza na Leicester 'Foxes' kuhusu uhamisho wake.

Pamoja na kuanza mechi nane kati ya 14,  alizocheza Ligi Kuu England msimu uliopita bado Elneny amekataa kujiunga na Leicester.

Elneny anafurahi maisha ya London tangu aliponunuliwa kwa pauni 5milioni kutoka FC Basel mwezi Januari.

Pamoja na uamuzi huo wa kiungo huyo  kubaki  Emirates bado atakuwa na nafasi ndogo ya kucheza kutokana na Gunners kuwa na nyota wa nafasi yake Francis Coquelin, Aaron Ramsey, Granit Xhaka na Alex Oxlade-Chamberlain.