Dogo wa Julio azidi kunoga

Muktasari:

  • Super amejiunga na timu hiyo akitokea Al Gharafa ya Qatar mara baada ya kufuzu kwenye majaribio.

SASA nenda kacheze anga za Julio usikie maneno yake ya shombo. Ndio, yule mtoto wa Kocha wa Dodoma, Jamhuri Kihwelu, Super amefungua ukurasa upya wa maisha yake ya soka baada ya kujiunga na Varzim ya Ligi Daraja la Kwanza kule ‘LigaPro’, Ureno.

Super amejiunga na timu hiyo akitokea Al Gharafa ya Qatar mara baada ya kufuzu kwenye majaribio.

“Nimesaini mkataba wa miaka mitatu, kila kitu Mungu alinisaidia kwa sababu kama ni ujanja na uwezo wa kucheza sio peke yangu mwenye nao,” alisema Super.

Super ameungana na Mtanzania mwingine, Orgeness Mollel wa Famalicao, ambaye naye ni mchezaji wa timu daraja la kwanza nchini humo.