Dilunga azidi kuzamisha jahazi la Njombe Mji

KIUNGO wa Mtibwa Sugar, Hassan Dilunga amezidi kulizamisha jahazi la Njombe Mji, baada ya kuifunga bao moja ambalo limedumu mpaka mpira unamalizika.

Bao hilo limezidi kuidhoofisha Njombe Mji kutokana na timu hiyo iliyokuwa ikihitaji ushindi ili kujiweka sehemu nzuri, kwani hivi sasa inashika nafasi 16 wakiwa na pointi 22 katika michezo 29 waliyocheza.

 Kutokana na matokeo hayo, Njombe anamuombea matokeo mabovu Ndanda (pointi 23) itakayocheza na Mwadui, ili wasiwe na gepu kubwa la pointi  wakati huo huo Majimaji nao ambao wanashika nafasi ya 29 wakiwa na pointi 24, wao wakijipanga kutafuta sare au ushindi katika mchezo wao dhidi ya Majimaji.