Dili la Mtogo Simba,Yanga limekuwa dirisha aisee!

Muktasari:

  • Iko hivi, ni kweli timu hizo zilikuwa zinamwania mchezaji huyo vikosini mwao lakini kwa sasa timu hizo zimesimamisha mawasiliano.

Dar es Salaam; Mpango wa Mtogo wa Wolaitta Dicha ya Ethiopia, Arafat Djako kutua kwenye klabu za Simba na Yanga 'dili' hilo huenda likawa dirisha kama vijana wa mjini wanavyopenda kuzungumza.
Iko hivi, ni kweli timu hizo zilikuwa zinamwania mchezaji huyo vikosini mwao lakini kwa sasa timu hizo zimesimamisha mawasiliano.
Amesema, kutokana na ukimya wao huenda akafanya mpango wa kwenda Misri ambako kuna timu moja inayomuhitaji.
"Mpaka sasa sina uhakika wa kuja huko naangalia 'dili' lingine nimepata nchini Misri. Naona kama jamaa wamekaa kimya katika kipindi hiki lakini kama kutakuwa na jipya mtajua tu,"amesema Djako.
Djako mshambuliaji wa Wolaitta timu za Simba na Yanga zimemjua baada ya kufanya vizuri katika kikosi chake hicho alipokuja Tanzania kucheza Kombe la Shirikisho Afrika.
Walicheza na Yanga Uwanja wa Taifa wakafungwa mabao 2-0 na ugenini Wolaitta walishinda bao moja ambalo lilipachikwa na Djako.