Diego Costa aanza kujinadi kwa Mourinho

London, England. Mshambuliaji  Diego Costa amekumbushia simu ya kocha wa Manchester United, Jose Mourinho aliyompigia muda mfupi baada ya kocha wake, Antonio Conte kumwambia hayuko katika mipango yake Chelsea.

Mshambuliaji  huyo wa Hispania kwa sasa yuko Brazil alionyeshwa mlango wa kutokea na Conte na sasa anahangaika kusaka timu ya kucheza kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Costa bado anahaha aweze kuondoka jumla Blues hatua inayomkwamisha kutengeneza utaratibu mwingine

Alisema kuwa baada ya kutemwa alipata simu nyingi ikiwemo ya Mourinho, lakini hata hivyo hakusema kama alimwambia aende Old Trafford ama la.

Hata hivyo, baada ya Chelsea kufungwa na Arsenal  katika mchezo wa Ngao ya Jamii na mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu dhidi ya Burnley kumekuwa na kelele za mashabiki wakimtaja Costa arudishwe kundini.