Diamond, Wema kivutio msiba wa Mzee Majuto

Dar es Salaam. Wasanii Wema Sepetu na Diamond wamegeuka kivutio katika shughuli za kumuaga mwili wa Mzee Majuto zilizofanyika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Diamond aliwasili katika viwanja hivyo akiwa na Meneja wake Salaam na Babu Tale, mbali ya kushirki kuaga pia alibeba jeneza la Mzee Majuto jambo liliwavutia na wengine kushiriki tukio hilo.
Baada ya kumaliza alielekea katika gari lake za rangi ya silva huku akiwa amezungukwa na walinzi takribani wanne waliovalia nguo nyeusi
Wakati akiwa anaelekea huko baadhi ya waombolezaji walimfuata nyuma wakiwemo walioshiriki kubeba naye jeneza na kupiga naye picha.
Kwa  wale ambao hawakuambulia kumpata walipiga picha kwenye gari lake ambalo lilisimama viwanjani hapo takribani nusu saa kabla halijaondoka.
Naye Wema aliyekuwa amevalia gauni la rangi ya maziwa hali ilikuwa hivyo hivyo kwa mashabiki kumzingira kupiga naye picha kuanzia anatoka ukumbini hadi kuelekea alipokuwa amepaki gari.
Tofauti na wasanii wengine walikubali kuzungumza na wanahabari namna walivyopokea taarifa za msiba huo, Wema alikataa akizungumza chochote.