Diamond, Kiba mambo ni moto

Muktasari:

  • Mbali na Diamond aliyenyakua tuzo mbili na Kiba aliyebeba moja, wengine waliong’ara katika tuzo hizo zilizotolewa Machi 17 ni Vanessa Mdee na Darassa.

WAIMBAJI wenye upinzani mkubwa katika muziki wa kizazi kipya nchini, Diamond na Ali Kiba ni kati ya wasanii wa Kibongo waliofunika nchini Uganda kupitia Tuzo za Muziki za Hipipo 2018.

Mbali na Diamond aliyenyakua tuzo mbili na Kiba aliyebeba moja, wengine waliong’ara katika tuzo hizo zilizotolewa Machi 17 ni Vanessa Mdee na Darassa.

Diamond alitwaa Tuzo ya Video Bora ya Afrika kupitia wimbo wa ‘Eneka’ na kubeba ya Wimbo Bora wa Mwaka kupitia ‘Merry You’ aliomshirikisha Mmarekani Ne-Yo.

Kiba alishinda tuzo ya Wimbo Bora wa Tanzania kupitia ngoma yake ya ‘Seduce Me’, huku Muziki aliomshirikisha Ben Po ukimbeba Darasa katika tuzo ya Wimbo Mkali wa Afrika Mashariki na Vannesa akishinda tuzo ya Msanii Bora wa Kike wa Afrika Mashariki.