Desemba ya mshikemshike England

Tuesday November 14 2017

 

LONDON, ENGLAND. SIKU zinakwenda kasi si mchezo. Kufumba na kufumbua, mara Desemba hiyo
inafika, mwezi mgumu kabisa kwenye mikikimikiki ya Ligi Kuu England.
Mwanaspoti linakutelea ratiba ya Desemba kwa klabu za Top Six kwenye msimamo
wa Ligi Kuu England kuona nani mwenye shughuli pevu na nani atakuwa
anakenua tu katika mechi hizo wakati ikikaribia Krismasi.

Arsenal – mechi 8

Kasheshe. Ile Desemba tu inaingia, Arsenal itakuwa na kibarua nyumbani wakati itakapowakaribisha Manchester United kwenye Uwanja wa Emirates, Desemba 2. Siku tano baadaye, watashuka tena kwenye uwanja huo kumenyana na BATE Borisov, kabla ya kukipiga na Southampton, West Ham United, Newcastle United, Liverpool, Crystal Palace na West Brom.

RATIBA YA DESEMBA

Des 2 vs Man United (nyumbani)

Des 7 vs BATE borisov (nyumbani)

Des 10 vs Southampton (ugenini)

Des 13 vs West Ham (ugenini)

Des 16 vs Newcastle (nyumbani)

Des 22 vs Liverpool (nyumbani)

Des 28 vs Crystal Palace (ugenini)

Des 31 vs West Brom (ugenini)

Chelsea – mechi 8

Kocha, Antonio Conte anakuna kichwa kwa sasa akitafakari namna ya kubadili kibao na kuifanya timu yake kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu England. Desemba inakuja na hakika huo ni mwezi mgumu kwa kila timu ya England, huku Chelsea wao wakionekana kutokuwa na ratiba ngumu sana inayoonekana kuwababe.

RATIBA YA DESEMBA

Des 2 vs Newcastle (nyumbani)

Des 5 vs At.Madrid (nyumbani)

Des 9 vs West Ham (ugenini)

Des 12 vs Huddersfield (ugenini)

Des 16 vs Southampton (nyumbani)

Des 23 vs Everton (ugenini)

Des 26 vs Brighton (nyumbani)

Des 30 vs Stoke City (nyumbani)

Liverpool – mechi 8

Kikosi hicho cha Jurgen Klopp kinapambana na hali yake licha ya kucheza hivyo kwenye mwezi Oktoba. Kwa sasa inajaribu kurudi kwenye makali yake, huku ratiba yao ya Desemba ikiwa kitu muhimu kabisa katika kubadili sura ya mwendo wao katika ligi ya msimu huu ili kupambana kuwamo kwenye Top Four.

RATIBA YA DESEMBA

Des 2 vs Brighton (ugenini)

Des 6 vs Spartak Moscow

(nyumbani)

Des 10 vs Everton (nyumbani)

Des 13 vs West Brom (nyumbani)

Des 17 vs Bournemouth (ugenini)

Des 22 vs Arsenal (ugenini)

Des 26 vs Swansea City (nyumbani)

Des 30 vs Leicester City (nyumbani)

Man City – mechi 8

Manchester City inafunika kila njia kwa wakati huu na kocha Pep Guardiola anataka kuendelea kutamba zaidi basi, anapaswa kuendelea kufanya kweli kwenye mwezi Desemba ambao, kimsingi ndiyo mgumu zaidi kwenye Ligi Kuu England kwa sababu kunakuwa na mechi nyingi zinazocheza ndani ya siku chache. Moja ya mechi zake za Desemba, Guardiola atakuwa na kazi ya kwenda kuvaana na mpinzani wake wa karibu, Jose Mourinho na kikosi chake cha Manchester United huku akiwa na mechi ngumu ya ugenini huko Ukraine siku nne kabla.

RATIBA YA DESEMBA

Des 3 vs West Ham (nyumbani)

Des 6 vs Shakhtar Donetsk

(ugenini)

Des 10 vs Man United (ugenini)

Des 13 vs Swansea City (ugenini)

Des 16 vs Tottenham (nyumbani)

Des 23 vs Bournemouth (nyumbani)

Des 27 vs Newcastle United

(ugenini)

Des 31 vs Crystal Palace (ugenini)

Man United – mechi 8

Ni mwezi wa shughuli kweli kweli kwa kocha Jose Mourinho katika kikosi chake cha Manchester United. Katika mwezi wa Desemba, Man United ya Mourinho itakabiliwa na mechi kadhaa ngumu ikiwamo kuwavaa Arsenal na mahasimu wao Man City, ambao mechi yao itakuwa na upinzani mkali kweli kweli kama wataendelea kufukuzana kama ilivyo kwa sasa kwenye msimamo wa ligi hiyo. Man City inaiongoza Man United kwa tofauti ya pointi nane katika msimamo wa Ligi Kuu England.

RATIBA YA DESEMBA

Des 2 vs Arsenal (ugenini)

Des 5 vs CSKA Moscow (nyum bani)

Des 10 vs Man City (nyumbani)

Des 13 vs Bournemouth (nyumbani)

Des 17 vs West Brom (ugenini)

Des 23 vs Leicester City (ugenini)

Des 26 vs Burnley (nyumbani)

Des 30 vs Southampton (nyumbani)

Tottenham Hotspur

Kwa kikosi cha Mauricio Pochettino mechi ngumu kwa Desemba itakuwa ile ya uwanjani Etihad watakwenda kupambana na wenyeji wao, Manchester City. Kama Spurs watafanikiwa kushinda mechi hiyo dhidi ya Man City wanaopewa nafasi kubwa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, basi Desemba haitakuwa ngumu sana kwa Kocha Pochettino kwani mechi nyingine zilizobaki hazionekani kuwa na ugumu sana. Mechi nyingine ngumu itakuwa dhidi ya wenzake wa kutoka jiji la London, West Ham United.

RATIBA YA DESEMBA

Des 2 vs Watford (ugenini)

Des 6 vs Apoel Nicosia (nyumbani)

Des 9 vs Stoke City (nyumbani)

Des 13 vs Brighton (nyumbani)

Des 16 vs Man City (ugenini)

Des 23 vs Burnley (ugenini)

Des 26 vs Southampton (nyumbani)

Des 31 vs West Ham (nyumbani)