Dembele, Coutinho waitoa macho Barca

Friday August 11 2017

Madrid, Hispania. Barcelona itashindwa kuinasa saini ya mshambuliaji wa Liverpool, Mbrazil Philippe Coutinho na Ousmane Dembele kwa wakati mmoja kwa kuwa fedha iliyotumika kumuuza Neymar hawezi kununua wachezaji hao wawili kwa mpigo.

Dembele anayekipiga, Borussia Dortmund yuko katika mipango ya kutua Camp Nou lakini inaelezwa kuwa mpango huo huenda ukazimika lakini endapo kati ya mmoja wao atasajili ambaye ni kipaumbele.

Coutinho anatakiwa na klabu hiyo ya Nou Campa kuziba pengo la Neymar lakini kocha wake, Jurgen Klopp ametia ngumu mchezaji huyo kuondoka.

Wakati huohuo; Baada ya kuzidi kwa uvumi wa kuondoka, Bosi wa klabu ya Borussia Dortmund, Peter Bosz amemsimamisha mazoezi staa wake, Ousmane Dembele.

Bosi alisema kuwa mchezaji huyo anatakiwa na Barcelona na ndiyo maana hakutaka kumweka katika mazoezi kwa kuwa akili yake haitakuwa uwanjani.

Pamoja na kuwepo kwa taarifa za Barca kumtaka, pia kumekuwepo na taarifa nyingine kwamba Dortmund imechomoa ofa hiyo ya Barca kwenda Nou Camp.