De Gea kumrudisha Cristiano Ronardo Man Utd

Muktasari:

Imefahamika kwamba kocha wa Manchester Jose Mourinho ana shauku kubwa ya kukuatana na Ronaldo kwa mara nyingine akiamini kwamba atamsaidia katika harakati zake za kusaka ubingwa wa Ligi Kuu England msimu unaokuja.

MANCHESTER, ENGLAND. TAARIFA zilizopo ni kwamba uongozi wa Manchester United unadaiwa kuwa upo tayari kumruhusu David de Gea ajiunge na Real Madrid lakini iwapo watabadilishana na Cristiano Ronaldo katika dirisha la usajili linalokuja. 

Imefahamika kwamba kocha wa Manchester Jose Mourinho ana shauku kubwa ya kukuatana na Ronaldo kwa mara nyingine akiamini kwamba atamsaidia katika harakati zake za kusaka ubingwa wa Ligi Kuu England msimu unaokuja.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na habari kwamba Madrid inafanya jitihada za kuhakikisha inamchukua De Gea na  kwamba nyota huyo wa Hispania ana shauku kubwa ya kutua katika jiji la Madrid.

Taarifa nyingine zinasema Mourinho yupo tayari kumtoa Paul Pogba kama njia nyingine ya kushawishi upatikanaji wa Ronaldo raia wa Ureno Manchester.

Ronaldo amewahi kuishi kwa miaka sita akiwa katika kikosi cha Old Trafford kabla ya kuhamia Bernabeu  mwaka 2009  kwa kiasi cha Pauni 80milioni.