Dauda arejeshwa tena TFF

Thursday August 10 2017Shaffih Dauda

Shaffih Dauda 

By Matereka Jalilu,Dodoma

KAMATI ya rufani ya uchaguzi wa TFF iliyoketi juzi Jumanne mjini hapa, imewarejesha baadhi ya wagombea waliokuwa wameenguliwa awali wakiwemo wanne waliotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa. Kikao hicho kilichofanyika Ukumbi wa St. Gasper kilifanya uamuzi mgumu.

Jumla ya rufani zilizowasilishwa mezani kwao ni tano ambazo zilikuwa zinahusu kuanza kampeni mapema na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa huku rufani nyingine ikiwa ni uzoefu wa kusimamia mpira iliyomhusu Mwenyekiti wa Chama cha soka Singida, Mussa Sima.

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Keneth Mwenda alisema; “Kamati yetu baada ya kupitia maelezo na nyaraka zote zilizowasilishwa mbele yetu tumejiridhisha kuwa warufani wote hawakupewa fursa ya kuhojiwa.”

Baadhi ya waliorejeshwa kwenye mchakato ni Shaffih Dauda (Dar es Salaam), Benista Lugola (Shinyanga), na Elias Mwanjala kutoka Mbeya