Ajib, Tambwe warudi kumuua Mnyama Simba

Muktasari:

  • Wachezaji hao ambao walikuwa na matatizo mbalimbali ni pamoja na Ibrahim Ajib, Amiss Tambwe, Andrew Vincent 'Dante'  na Thabaan Kamusoko.

KIKOSI cha  Yanga, kinaendelea na mazoezi yake kama kawaida kwenye Uwanja wa Highland uliopo karibu kabisa milima ya Uluguru mkoani Morogoro na habari nzuri ni kwamba, wachezaji wao ambao hawakuwa na timu kwa kipindi kirefu, wamejiunga na wenzao na kuongeza mzuka wa kuwafunga Simba Aprili 29.

Wachezaji hao ambao walikuwa na matatizo mbalimbali ni pamoja na Ibrahim Ajib, Amiss Tambwe, Andrew Vincent 'Dante'  na Thabaan Kamusoko.

Ambapo jana Jumanne, walifanya mazoezi makali chini ya makocha wao, Mzambia Noel Mwandila pamoja na Shadrack Nsajigwa ambao walionekana hawataki masihara na kuwa wakali muda wote huku wakiwataka wachezaji kutekeleza majukumu yote.

Kikosi hicho ambacho kitaiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi, kilianza mazoezi yake saa tisa jioni na kumaliza masaa mawili baadaye.