DSJ waliamsha dude shindano la utangazaji

Muktasari:

  • Katika mashindano hayo, DSJ walikuwa wanatafuta watangazaji bora kwenye vipengele vya michezo, burudani, vipindi maalum na usomaji wa habari.

Dar es Salaam.Wanafunzi  wa chuo cha uandishi wa habari cha Dar es Salaam School of Journalism (DSJ), waliamsha dude katika  mashindano ya utangazaji.

Katika mashindano hayo, DSJ walikuwa wanatafuta watangazaji bora kwenye vipengele vya michezo, burudani, vipindi maalum na usomaji wa habari.

Walioibuka kidede ni Jabir Hamis katika Michezo, Matlida Peter katika  Burudani, Clement  Robert katika vipindi maalum na kwa upande wa Habari ni Florian Rutahiwa.

Uamuzi wa jaji mkuu, Grace Kingalame aliyekuwa akisaidiwa na Godwin Mawanja yaliamua washindi kwenye vipengele vilivyoshindaniwa.

Waliokuwa wanashindanishwa katika fainali hiyo kwa upande wa  michezo ni Jabir Hamis 'kiungo mnyumbulifu', habari ni Dina Mgana, Florian Rutahiwa, Sheila Abdul, Godbless Gaspar, Itika Francis

Burudani ni Ally Chiwaga, Raymond Casto, Johnson Kayombo, Matilda Peter, Abdan Twamaenk, kipindi maalum ni Clement  Robert, Maria Alphonce.