Cristiano Ronaldo aanzishiwa zengwe

Muktasari:

Licha ya kupasia sana nyavuni na kuibeba klabu yake hasa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ronaldo ameingia matatani baada ya kutuhumiwa kumnyanyasa kijinsia, mrembo Erika Canela.

SUPASTAA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameingia kwenye kumi na nane za mrembo wa Kibrazili.

Licha ya kupasia sana nyavuni na kuibeba klabu yake hasa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ronaldo ameingia matatani baada ya kutuhumiwa kumnyanyasa kijinsia, mrembo Erika Canela.

Canela ametishia kumshitaki mahakamani Ronaldo kwa kumfanya kupitia kwenye kipindi kigumu wakati alipomtema.

“Aliniacha kwenye mazingira magumu na kunipa msongo wa mawazo, pia alinisababishia aibu kubwa kwa watu waliokuwa wakifahamu uhusiano wetu,” alilalamika Canela.