Coutinho atuliza mzuka Liverpool

Monday November 13 2017

London, England. Kiungo nyota wa timu ya

Liverpool, Philippe Coutinho amesisitiza ana furaha ndani ya klabu hiyo.

Coutinho alisema licha ya jaribio la kutaka kujiunga na Barcelona kukwama, lakini ana furaha kubaki Liverpool.

Alisema Liverpool inacheza katika moja ya Ligi Kuu zenye ushindani mkubwa duniani, hivyo hana sababu ya kutokuwa na furaha.

Mchezaji huyo alisema anataka kujikita katika timu ya taifa ya Brazil ambayo imekata tiketi kucheza fainali za Kombe la Dunia mwakamo.

“Nacheza katika moja ya klabu kubwa duianim, nina furaha kubaki hapa kucheza katika klaniu kubwa,” alisema Coutinho.

Liverpoo iliweka ngumu kumtoa Coutinho mara tatu, licha ya kuweka mezani fedha za maana kumng’oa katika majira ya kiangazi msimu uliopita.

Barcelona inamtaka mchezaji huyo kwenda kuziba pengo la Neymar aliyejiunga na Patis Saing Germaini (PSG).