Conte kurudi kuinoa Italia

Muktasari:

  • Italia imeshindwa kufuzu fainali hizo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 60 baada ya kutolewa na Sweden kwenye mechi za mchujo.

RAIS wa Shirikisho la soka la Italia, Carlo Tavecchio amethibitisha kwamba kocha wa Chelsea, Antonio Conte ana nafasi kubwa ya kuwa kocha wa kikosi cha Azzurri.

Timu ya soka ya taifa ya Italia kwa sasa haina kocha baada ya Gian Piero Ventura kufutwa kazi hivi karibuni kufutia timu hiyo kushindwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 zitakazofanyika Russia.

Italia imeshindwa kufuzu fainali hizo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 60 baada ya kutolewa na Sweden kwenye mechi za mchujo.

Mara ya mwisho Italia kushindwa kukamata tiketi ya fainali za Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 1958, zilizofanyika Sweden. Mipango ya Italia kwenye michuano mikubwa kwa sasa ni kusubiri mikikimikiki ya Euro 2020.