Adili wa Coastal akaribia Njombe Mji

Muktasari:

Hata hivyo, licha ya tetesi hizo, Kabange hakutaka kuweka wazi usajili huo na kusisitiza, bado ni mapema kufanya hivyo mpaka watakapokamilisha taratibu zote.

KLABU ya Njombe Mji ya Njombe, inafanya juu chini kuhakikisha inamsajili kiungo mshambuliaji wa Coastal United, Adil Nassor kwenye dirisha dogo kwa ajili ya kuiongezea nguvu timu yao.
Adil ambaye amebakiza miezi sita na Coastal inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, tayari ameshaanza mazungumzo ya awali na Njombe inayonolewa na kocha, Mlage Kabange.
Hata hivyo, licha ya tetesi hizo, Kabange hakutaka kuweka wazi usajili huo na kusisitiza, bado ni mapema kufanya hivyo mpaka watakapokamilisha taratibu zote.
"Siwezi kutaja mchezaji yeyote kwa sasa mpaka nitakapo kamilisha taratibu zote, kama unavyojua kuna timu nyingine wakijua jina tu,  basi  zinawahi mapema,"alisema Kabange ambaye pia ni mwanachama wa klabu ya Simba.