Class, Msauzi kumaliza ubishi kesho

Muktasari:

Mabondia hao watapanda ulingoni kesho mchana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Mabondia Ibrahim Class na Koo's Sibiya wamepima uzito na afya tayari kwa pambano lao la ubingwa wa dunia wa GBC litakalopigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Class alipaswa kupunguza kilo gramu mbili, alifanikiwa katika zoezi la kupima uzito ambapo alipata kilo 58.5 sawa na mpinzani wake zoezi ambalo lilishuhudiwa pia na viongozi kutoka GBC.

Kwa nyakati tofauti mabondia hao walitambia kila mmoja akijinasibu kuondoka na taji hilo ambalo Class analitetea.

Pambano hilo litaanza saa 8 mchana likitanguliwa na mapambano mengine tisa.