Chollo: Ligi Daraja la Kwanza ya watu fiti

Dar es Salaam. Beki wa Dodoma FC, Masoud Nassor 'Chollo' ametoboa siri jinsi wachezaji wa Daraja la Kwanza wanavyotamani ajira za Ligi Kuu jambo linalochangia ushindani mkali katika ligi hiyo.

Chollo nahodha wa zamani wa Simba, alisema kawaida kujenga ni kugumu kuliko kubomoa, akimanisha baadhi ya wachezaji wa Ligi Kuu wanaoshindwa kujituma na kulinda heshima ya sehemu zao za kazi.

"Ukisikia wachezaji wapo fiti basi na hawa wa ligi daraja la kwanza, wanajituma wanatamani waonekane na mabosi watakaowapa nafasi ya kucheza Ligi Kuu Bara," alisema.

Ameeleza heshima anayoipata ndani ya kikosi hicho inatokana na kuepuka ubaguzi wa umri na kidini anachokifanya ni wote kuwafanya wapo sawa.

"Ukitaka kuleta mgawanyiko kwenye timu basi aanza kuweka makundi ya umri na dini, hakuna kitakachofanyika, najishusha kwao wapo huru kujifunza lolote wanalolitaka,"alisema.