Chilunda apima afya kutambulishwa

Mshambuliaji huyo amekuwa na msimu wa mafanikio akiwa na klabu ya Azam
Tenerife, Hispania. Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Shaaban Idd Chilunda amefanyiwa vipimo vya afya jana Alhamisi na  Ijumaa atatambulishwa rasmi katika klabu yake mpya ya CD Tenerife.
Mshambuliaji huyo mpya amesaini mkataba wa miaka miwili, atatambulishwa saa 11:00 asubuhi na mkurungezi wa ufundi CD Tenerife, Alfonso Serrano kwenye ukumbi wa Hatusa (Red Volkswagen Canarias), ambao ni wadhamini wakuu wa CD Tenerife.
Chilunda amefanyiwa vipimo vya afya katika Hospitali ya Rambla leo na kesho Ijumaa atajiunga na wachezaji wenzake saa 6:00 mchana katika kituo cha Javier Pérez Sports Center, mazoezi hayo yatasimamiwa na kocha pamoja benchi la ufundi la CD Tenerifa.
Akizungumza wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Tenerife North Airport, mshambuliaji huyo wa Tanzania alisema "ni jambo zuri kwake kujiunga na Tenerife yupo tayari kuisaidia timu kufanya vizuri."