Chelsea yasalimu amri kwa Diego Costa sasa kwa hasara

London, England. Uongozi wa Chelsea umeamua kumuuza kwa hasara mshambuliaji wake, Diego Costa baada ya kugomea kujiunga na kikosi hicho katika msimu mpya Ligi Kuu England.

Kutokana na sakata hilo kuendelea tangu ligi hiyo ilipoanza, uongozi umeamua kumuuza kwa Atletico Madrid, klabu aliyokuwa anatazamiwa kwenda kujiunga baada ya kutokea msuguano na kocha Antonio Conte.

Tayari Chelsea imetangaza dau la Pauni 20 milioni ikilinganishwa na dau la Pauni 50 milioni alilosajiliwa na mabingwa hao wa England walipomchukua kutoka Atletico Madrid.