Chelsea yampa Diego Costa masharti manne magumu iwapo anataka kwenda Atletico

Muktasari:

  • Taarifa iliyotolewa leo Jumanne na uongozi wa klabu hiyo imeeleza kwamba Chelsea imempa masharti manne kabla ya kumuuza Atletico Madrid.

Klabu ya Chelsea imempa masharti manne mchezaji wake, Diego Costa ambaye amegoma kurejea London ili kujiunga na kikosi hicho.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne na uongozi wa klabu hiyo imeeleza kwamba Chelsea imempa masharti manne kabla ya kumuuza Atletico Madrid.

Mambo aliyoelezwa ni kama yafuatayo; kurudi London, kujiunga mazoezini na wenzake, aimarishe kiwango chake kwenye mechi na aongeze juhudi kuwapo kikosi cha kwanza.